Kombe la Dunia 2026

IQNA

IQNA-Kituo cha Kiislamu cha Al-Azhar cha Kupambana na Misimamo Mikali kimeonyesha wasiwasi mkubwa kufuatia ongezeko la matamshi ya chuki na chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) wakati wa michuano ya Kombe la Dunia ya mwaka 2026.
Habari ID: 3482527   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/23

IQNA-Afisa mwandamizi wa Harakati ya Kiislamu ya Mapambano ya Palestina, Hamas, ametoa pongezi za dhati kwa Uhispania kufuatia ushindi wake baada ya mechi ngumu katika fainali ya Kombe la Dunia la FIFA la mwaka 2026, akielezea mafanikio hayo kuwa ni chanzo cha furaha kwa watu wa Palestina na wafuasi wote wa haki, huku akibainisha kuwa ushindi huo ni pigo hasa kwa utawala wa Kizayuni wa Israel na wafadhili wake.
Habari ID: 3482512   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/20

IQNA – Gavana wa Dakahlia, nchini Misri, amemtunuku nakala ya Qur’ani Tukufu Imam Ashour, mchezaji wa timu ya taifa ya Misri na klabu ya Al-Ahly, ikiwa ni ishara ya kutambua juhudi zake katika Kombe la Dunia la mwaka 2026.
Habari ID: 3482508   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/19

IQNA – Mashindano ya Kombe la Dunia la 2026 yanafanyika kote Amerika Kaskazini, lakini “sauti” kuu ya michuano hiyo inayoimbwa bila shaka ni ile ya kuunga mkono Palestina.
Habari ID: 3482439   Tarehe ya kuchapishwa : 2026/07/04